http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html
Showing posts with label Polisi Tanzania inamshikilia baba aliyemtoa kafara mwanawe kwa shilingi milioni tano. Show all posts
Showing posts with label Polisi Tanzania inamshikilia baba aliyemtoa kafara mwanawe kwa shilingi milioni tano. Show all posts

Monday, May 13, 2019

Polisi Tanzania inamshikilia baba aliyemtoa kafara mwanawe kwa shilingi milioni tano

Polisi Tanzania inamshikilia baba aliyemtoa kafara mwanawe kwa shilingi milioni tano
Polisi mkoani Mbeya nchini Tanzania, inashikilia watu wawili kwa kuhusika na mauaji ya mtoto wa miaka sita Rose Japhet, aliyeuawa kutokana na imani za kishirikina.

Kamanda wa Polisi katika mkoa wa Mbeya Ulrich Matei amesema uchunguzi wao umebaini kuwa mtoto huyo aliuawa tarehe 3 mwezi huu kwa kunyongwa na baadhi ya viungo vyake kunyofolewa.

Miongoni mwa watuhumiwa wa mauaji hayo ya kinyama ametajwa kuwa ni Japhet Nguku, baba mzazi wa mtoto huyo wa miaka 6. Inaelezwa kuwa chanzo cha mauji haya ni tamaa ya fedha, na baba wa msichana huyo alikubali kumuua mtoto wake ili kupata Shilingi Milioni tano za Tanzania.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akishiriki mazishi ya watoto waliochinjwa Njombe