http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html
Showing posts with label Japan yaionya Marekani kuhusu vitendo vya utesaji wa askari wake kwa wakazi wa Okinawa. Show all posts
Showing posts with label Japan yaionya Marekani kuhusu vitendo vya utesaji wa askari wake kwa wakazi wa Okinawa. Show all posts

Thursday, April 18, 2019

Japan yaionya Marekani kuhusu vitendo vya utesaji wa askari wake kwa wakazi wa Okinawa

Japan yaionya Marekani kuhusu vitendo vya utesaji wa askari wake kwa wakazi wa OkinawaWaziri wa Ulinzi wa Japan ameitahadharisha Marekani kuhusiana na vitendo vya utesaji vya askari wa Kimarekani dhidi ya wakazi wa kisiwa cha Okinawa cha Japan.

Takeshi Iwaya ametoa onyo hilo kufuatia mauaji ya mwanamke mmoja raia wa Japan aliyeuawa na askari wa Marekani katika eneo hilo na kusema kuwa, ni lazima Washington idhibiti mienendo mibaya ya askari wake katika kisiwa cha Okinawa, sambamba na kuhitimisha hali ya ukosefu wa udhibiti kati ya askari hao. 

Aidha Waziri wa Ulinzi wa Japan amebainisha kwamba wakazi wa kisiwa hicho wana wasi wasi mkubwa kutokana na uwepo wa askari wa Kimarekani katika kisiwa hicho na amebainisha kwamba ili kuzuia matukio yanayotokana na utumiaji mabavu wa askari hao katika eneo hilo, kuna haja ya kuchukuliwa hatua madhubuti katika uwanja huo.

Askari wa Marekani walioko katika kisiwa cha Okinawa

Inafaa kuashiria kuwa, siku chache zilizopita askari mmoja wa Marekani mwenye umri wa miaka 32, alimuua mwanamke mmoja raia wa Japan katika kisiwa cha Okinawa kwa kumchoma kisu kisha naye akajiua.