http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html
Showing posts with label lafunga ofisi za kituo cha Aljazeera. Show all posts
Showing posts with label lafunga ofisi za kituo cha Aljazeera. Show all posts

Friday, May 31, 2019

Jeshi lawaonya waandamanaji, lafunga ofisi za kituo cha Aljazeera

Na Emmanuel Richard Makundi Imechapishwa 31-05-2019 Imehaririwa 31-05-2019 Saa 09:02

Watawala wa kijeshi nchini Sudan wanasema kuwa kambi za waandamanaji mjini Khartoum zimekuwa tishio kwa usalama wa taifa, wakati huu jeshi likiagiza kufungwa kwa ofisi za kituo cha habari cha Aljazeera.

media
Waandamanaji wa Sudan wakiwa na mabango katika moja ya maandamano yao ya hivi karibuni.
REUTERS/Umit Bektas

Katika taarifa waliyoitoa kupitia televisheni ya taifa, msemaji wa baraza la kijeshi amesema hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watu aliosema waharibifu.

Kwa miezi kadhaa sasa waandamanaji wameendelea kutia ngumu kutoka kwenye maeneo yanayozingira makao makuu ya jeshi wakishinikiza jeshi kukabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia.

"Eneo la maandamano limekuwa si salama na linahatarisha usalama wa taifa," alisema Jenerali Bahar Ahmed Bahar, mkuu wa jeshi mjini Khartoum.

Jeshi linasema magari maalumu ya kijeshi ya kikosi maalumu yamekuwa yakishambuliwa na mengine kuzuiliwa na waandamanaji kwenye eneo la maandamano.

Eneo hilo limekuwa kitovu cha vuguvugu la maandamano, ambayo yalishuhudia kuondoka madarakabi kwa rais Omar al-Bashir aliyeondolewa na jeshi mwezi uliopita, na tangu wakati huo wamekuwa wakitaka wanajeshi nao kukabidhi madaraka kwa raia.