http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html
Showing posts with label Waziri Mkuu wa Sri Lanka akiri kwamba vyombo vya upelelezi vya nchi yake ni dhaifu. Show all posts
Showing posts with label Waziri Mkuu wa Sri Lanka akiri kwamba vyombo vya upelelezi vya nchi yake ni dhaifu. Show all posts

Wednesday, April 24, 2019

Waziri Mkuu wa Sri Lanka akiri kwamba vyombo vya upelelezi vya nchi yake ni dhaifu

Waziri Mkuu wa Sri Lanka akiri kwamba vyombo vya upelelezi vya nchi yake ni dhaifu
Waziri Mkuu wa Sri Lanka, Ranil Wickremesinghe amekiri kwamba vyombo vya intelijensia vya nchi yake ni dhaifu, kutokana na miripuko ya kigaidi ya hivi karibuni katika mji mkuu wa nchi hiyo Colombo.

Wickremesinghe ameyasema hayo leo akizungumzia miripuko ya hivi karibuni ya kigaidi mjini Colombo na kuongeza kwamba licha ya kwamba awali serikali ya India ilikuwa imeipatia Sri Lanka taarifa za kiitelijensia kuhusiana na hatari ya kujiri hujuma hizo, lakini maafisa wa upelelezi wa nchi hiyo walishindwa kuzifanyia kazi kwa wakati. Waziri Mkuu wa Sri Lanka ameongeza kwamba, kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana hadi sasa, wahusika wa mashambulizi hayo ni kundi moja la raia wa nchi hiyo wenye mahusiano na pande za kigeni.

Idara ya upelelezi nchini Sri Lanka ambayo inalaumiwa kwa uzembe

Jumapili iliyopita, ya tarehe 21 Aprili kulijiri miripuko kadhaa ya kigaidi katika makanisa na hoteli kadhaa mjini Colombo ambapo kwa akali watu 359 waliuawa na wengine zaidi ya 500 kujeruhiwa. Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) limetangaza kuhusika na hujuma hiyo.

Wakati huo huo Naibu Waziri wa Ulinzi wa Sri Lanka amesema kuwa, watu wawili miongoni mwa waliohusika na miripuko ya mabomu ya siku ya Jumapili iliyopita mjini Colombo walikuwa ni wanafunzi wawili waliosomea Uingereza na Australia. Ruwan Wijewardene amesema kuwa watu wanane kati ya waliohusika na hujuma hiyo tayari wametambuliwa ambapo wawili kati yao ni wanafunzi wawili waliosomea nchi zilizotajwa. Aidha amesema kuwa hadi sasa idadi ya watu waliotiwa mbaroni kwa kuhusishwa na mashambulizi hayo imefikia 58.

Chnazo: parstoday.com