http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html
Showing posts with label Uturuki yaendeleza chokochoko. Show all posts
Showing posts with label Uturuki yaendeleza chokochoko. Show all posts

Thursday, June 13, 2019

Uturuki yaendeleza chokochoko, yatuma tena msafara wa jeshi kaskazini mwa Syria

Uturuki yaendeleza chokochoko, yatuma tena msafara wa jeshi kaskazini mwa Syria
Serikali ya Uturuki imetuma msafara mwingine wa kijeshi kaskazini mwa Syria kwa kisingizio cha kupambana na magaidi wa Kikurdi.

Duru za habari nchini Uturuki zimearifu kwamba, msafara huo wa jeshi unaojumuisha magari kadhaa ya deraya, askari watembeao kwa miguu na vifaru, uliowasili siku chache zilizopita katika eneo la mpakani la mkoa wa Hatay, kusini mwa Uturuki, uliingia kaskazini mwa Syria usiku wa Jumanne iliyopita. Baada ya kuwasili eneo hilo, msafara huo wa kijeshi ulielekea moja kwa moja katika mji wa Afrin wa mkoa wa Aleppo nchini Syria. Kadhalika duru za habari nchini Uturuki zimearifu kwamba msafara huo una lengo la kuimarisha uwezo wa kiulinzi wa jeshi la Uturuki katika uga wa operesheni za majeshi ya nchi hiyo yaliyoko kaskazini mwa Syria eneo la Afrin.

Uturuki yaendeleza chokochoko, yatuma tena msafara wa jeshi kaskazini mwa Syria
Msafara huo wa jeshi la Uturuki ukiingia ardhi ya Syria kinyume cha sheria

Kwa mara kadhaa serikali ya Damascus imekosoa uwepo wa majeshi ya Uturuki na Marekani katika ardhi yake kinyume cha sheria na imekwishawasilisha barua kadhaa kwa Umoja wa Mataifa kuhusu kadhia.

Mzozo wa Syria uliibuka mwaka 2011 baada ya makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Saudi Arabia, Marekani na washirika wao kuivamia nchi hiyo ya Kiarabu kwa lengo la kuleta mabadiliko katika eneo la Asia Magharibi kwa maslahi ya utawala khabithi wa Israel. Hata hivyo jeshi la Syria kwa kusaidiwa na washauri wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lilifanikiwa kulishinda kundi la kigaidi la Daesh (ISIS). Mbali na hayo jeshi la Syria linaendelea na juhudi za kuyasambaratisha mabaki ya kundi hilo nchini humo.

Chanzo: parstoday.com