http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html
Showing posts with label UN yapuuzilia mbali mkutano wa Manama wa kujadili mpango wa "Muamala wa Karne". Show all posts
Showing posts with label UN yapuuzilia mbali mkutano wa Manama wa kujadili mpango wa "Muamala wa Karne". Show all posts

Friday, May 31, 2019

UN yapuuzilia mbali mkutano wa Manama wa kujadili mpango wa "Muamala wa Karne"

UN yapuuzilia mbali mkutano wa Manama wa kujadili mpango wa
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa hautashiriki katika mkutano wa Kiuchumi uliopangwa kufanyika Manama mji mkuu wa Bahrain khususan kujadili mpango kwa jina la "Muamala wa Karne."

Farhan Haq, Msemaji wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa umoja huo hautashiriki katika mkutano huo wa Manama ambao unatarajiwa kufanyika kwa ajili ya kuwasilisha masuala ya kiuchumi kuhusu mpango wa Muamala wa Karne katika mzozo kati ya Israel na Palestina. Farhan Haq awali alitangaza pia kuwa Nicolay Mladenov Mratibu wa Masuala ya Mashariki ya Kati wa Umoja wa Mataifa amealikwa kushiriki mkutano wa Manama lakini akasema kuwa mratibu huyo hatoshiriki.

Hata hivyo baadaye Farhan Haq alisahihisha matamshi yake hayo na kusisitiza kuwa hakuna mwaliko kama huo. Mamlaka ya Ndani ya Palestina pia imesusia mkutano huo wa Manama.

Mkutano huo wa Marekani ulio dhidi ya Palestina umepangwa kufanyika tarehe 25 na 26 Juni mwaka huu huko Manama, Bahrain chini ya anwani "Muamala wa Karne." Kwa mujibu wa mpango huo, Quds Tukufu itakabidhiwa kwa utawala wa Kizayuni, wakimbizi wa Kipalestina wanaoishi katika nchi nyingine hawatakuwa na haki ya kurejea katika ardhi yao, na Palestina itamiliki tu ardhi zitakazosalia huko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Ghaza. Umoja wa Mataifa umepinga vipengee vya mpango huo wa hila uliopendekezwa na Marekani kwa kuwasilisha maazimio mbalimbali.

Quds Tukufu

Chanzo: parstoday.com