http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html
Showing posts with label Shari za Trump: Washington yazionya nchi za Ulaya kuhusu mkakati wao wa kutoishirikisha Marekani katika ulinzi. Show all posts
Showing posts with label Shari za Trump: Washington yazionya nchi za Ulaya kuhusu mkakati wao wa kutoishirikisha Marekani katika ulinzi. Show all posts

Thursday, May 16, 2019

Shari za Trump: Washington yazionya nchi za Ulaya kuhusu mkakati wao wa kutoishirikisha Marekani katika ulinzi

Shari za Trump: Washington yazionya nchi za Ulaya kuhusu mkakati wao wa kutoishirikisha Marekani katika ulinzi
Moja ya hitilafu kuu baina ya Marekani na nchi za Ulaya wakati huu wa urais wa Donald Trump huko Marekani, ni misimamo ya kukinzana ya pande mbili kuhusu siasa na miundo ya ulinzi ya Ulaya na nafasi ya shirika la kijeshi la nchi za Magharibi, NATO.

Suala hilo limepelekea nchi za Ulaya kuangalia upya siasa zao za kiulinzi na kufikiria kuwa na ulinzi huru wa bara Ulaya usioihitajia Marekani. Hata hivyo serikali ya Trump haifurahishwi hata kidogo na jambo hilo. Kama kawaida yake, Trump anatumia lugha ya vitisho hata kwa waitifaki wakuu wa Marekani yaani nchi za Ulaya na kuzionya kuwa Washington itachukua hatua kali dhidi yao iwapo zitaamua kutekeleza mipango yao huru ya kiulinzi na kisilaha na kuiweka pembeni Marekani. Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon imetishia kuwa, iwapo Umoja wa Ulaya utaendelea kutekeleza kivyake-vyake mipango yake ya ulinzi, Washington itazichukulia hatua nchi hizo. Hii ina maana ya kwamba Marekani inaweza kutumia masuala ya kibiashara na kisiasa kukabiliana na nchi za Ulaya iwapo zitaendelea kuchukua misimamo ya kujitegemea katika mambo yao ya kiulinzi bila ya kuishirikisha nchi ya nje ya Umoja wa Ulaya kama Marekani.

Ellen Lord, naibu waziri wa ulinzi wa Marekani, mwanzoni mwa mwezi huu wa Mei 2019 alimuandikia barua Federica Mogherini, Mkuu wa Siasa za Kigeni na Kiusalama wa Umoja wa Ulaya na kulalamikia siasa huru za umoja huo za kujitegemea katika sekta ya ulinzi na silaha. Barua hiyo ilizitishia nchi za Ulaya kuwa Washington itazichukulia hatua iwapo zitaendelea na mipango yake ya kiulinzi isiyoishirikisha Marekani. Katika barua hiyo, Ellen Lord aliandika: Umoja wa Ulaya umetekeleza kivyake-vyake mipango yake ya kiulinzi na kisilaha, suala ambalo linatishia ushirikiano wa kijeshi wa Marekani na Ulaya na ni kinyume na makubaliano ya NATO.

Shari za Donald Trump hazikubakisha mtu

Naibu huyo wa waziri wa ulinzi wa Marekani amesisitiza kuwa, kama Washington itajibu siasa hizo za Umoja wa Ulaya, basi majibu hayo hayatokuwa na mambo mazuri kwa washirika wa Washington huko Ulaya. Lord alidai kwenye barua yake hiyo kwamba: Sisi (Marekani) hatutaki tufike mahala tuchukue maamuzi kama hayo katika siku za usoni kwani uamuzi huo utakwenda sambamba na hasara ya mamilioni ya dola kwa mashirika ya kutengeneza silaha ya barani Ulaya.

Marekani imetoa vitisho hivyo katika hali ambayo tarehe 18 aprili 2019, Bunge la Ulaya lilipasisha mpango wa kuanzishwa mfuko maalumu wa kiulinzi wa Ulaya wenye thamani ya Euro bilioni 13 kwa ajili ya mwaka 2021 hadi 2027. Zaidi ya hayo, Washington inapinga masharti jumla yaliyoainishwa katika mpango wa ushirikiano wa kudumu unaojulikana kwa jina la PESCO. Kwa mujibu wa mpango huo, nchi 25 za Ulaya zimepanua miradi yao 34 ya silaha.