http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html
Showing posts with label Rais wa DRC Felix Tshisekedi kufanya ziara ya kwanza Tanzania. Show all posts
Showing posts with label Rais wa DRC Felix Tshisekedi kufanya ziara ya kwanza Tanzania. Show all posts

Thursday, June 13, 2019

Rais wa DRC Felix Tshisekedi kufanya ziara ya kwanza Tanzania

Na Emmanuel Richard Makundi

Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi Alhamisi ya wiki hii kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kwake atafanya ziara ya siku 2 nchini Tanzania ambapo atakutana kwa mazungumzo na mwenyeji wake rais wa Tanzania John Magufuli.


media
Rais wa DRC, Félix Tshisekedi wakati alipokuwa mjini Luanda, Angola, Februari 5, 2019.

Stringer/AFP


Rais Tshisekedi atawasili majira ya saa kumi jioni alasiri ambapo atapokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Tanzania.

Akiwa nchini Tanzania rais Tshisekedi anatarajiwa kutembelea bandari ya Dar es Salaam kabla ya baadae kukutana kwa mazungumzo na mwenyeji wale kwenye ikulu ya magogoni.

Ziara yake ni sehemu ya Kujitambulisha kwa rais Magufuli lakini pia kuendeleza ushirikiano wa kiuchumi, kibiashara na kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili jirani.

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka katika ikulu ya Kinshasa, rais Tshisekedi na mwenyeji wake wanatarajiwa kuzungumza kuhusu hali ya biashara baina ya nchi hizo mbili huku DRC ikiwa ni mtumiaji mkubwa wa bandari ya Dar es Salaam kupitishia mizigo yake.