http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html
Showing posts with label Rais Tshisekedi na Kabila wakutana kujadili uteuzi wa Waziri Mkuu. Show all posts
Showing posts with label Rais Tshisekedi na Kabila wakutana kujadili uteuzi wa Waziri Mkuu. Show all posts

Tuesday, April 23, 2019

Rais Tshisekedi na Kabila wakutana kujadili uteuzi wa Waziri Mkuu

Rais Tshisekedi na Kabila wakutana kujadili uteuzi wa Waziri Mkuu
Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaendelea kusubiri kwa hamu na shauku kubwa uteuzi wa Waziri Mkuu mpya, miezi kadhaa baada ya Felix Tshisekedi kuchukua mikoba ya Joseph Kabila kwenye uongozi wa nchi.

Wawili hao walikutana jana Jumatatu na kuzungumzia kuhusu nafasi ya Waziri Mkuu ambayo imesalia wazi, miezi minne baada ya uchaguzi wa urais uliompa ushindi Felix Tshisekedi na kuchukua hatamu za uongozi wa nchi.

Awali Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila walikuwa hawaelewani kufuatia mvutano wa kisiasa uliokuwa ukiikumba DRC na kisha baada ya uchaguzi wa urais wawili hao waliamua kufanya kazi kwa ushirikiano wakiwa katika muungano mmoja wa kisiasa.

Rais Tshisekedi na Joseph Kabila walikuwa hawajakutana kwa wiki kadhaa kutokana na ziara za kikazi za Tshisekedi. Lakini kwa pande zote mbili, wanahakikisha kuwa rais wa sasa na mtangulizi wake huzungumza mara kwa mara.

Felix Tshisekedi