http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html
Showing posts with label Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini afuta ratiba ya kushiriki sherehe kuadhimisha mazungumzo ya viongozi wa Korea mbili. Show all posts
Showing posts with label Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini afuta ratiba ya kushiriki sherehe kuadhimisha mazungumzo ya viongozi wa Korea mbili. Show all posts

Saturday, April 27, 2019

Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini afuta ratiba ya kushiriki sherehe kuadhimisha mazungumzo ya viongozi wa Korea mbili

Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini afuta ratiba ya kushiriki sherehe kuadhimisha mazungumzo ya viongozi wa Korea mbili
Kufuatia kushtadi mgogoro kati ya Korea mbili, Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini amefuta ratiba ya kushiriki katika sherehe za mwaka mmoja za kukutana na Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini, zilizokuwa zimepangwa kufanyika leo.

Jana Ko Min-jung, Msemaji wa Ikulu ya Rais wa Korea Kusini alisema kuwa, Rais Moon Jae-in hatoshiriki Jumamosi ya leo katika marasimu ya kutimia mwaka mmoja tangu viongozi hao wa nchi mbili walipokutana mwazi Aprili mwaka jana. Aidha Ko Min-jung aliongeza kwamba badala yake Rais Moon Jae-in atatuma tu ujumbe wa video kwende shere hizo. 

Weledi wa masuala ya kisiasa wamekutaja kuvunjika duru mbili za mazungumzo kati ya Rais Donald Trump wa Marekani na Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini huko mjini Hanoi, Vietnam, na pia hatua ya Korea Kusini kufanya maneva ya kijeshi na Marekani katika Rasi ya Korea kuwa ni mambo yaliyoifanya serikali ya Seoul kuchukua hatua hiyo.


Rais Moon Jae-in (kulia) alipokutana kwa mara ya kwanza na Kim Jong-un mwaka jana

Wakati huo huo, Alkhamisi iliyopita, serikali ya Pyongyang sambamba na kukosoa vikali hatua ya Korea Kusini na Marekani ya kufanya maneva ya pamoja ya kijeshi ya anga katika eneo hilo, ilitangaza kwamba, jeshi la Korea Kaskazini litatoa jibu muafaka kufuatia harakati hizo za kijeshi za jirani yake huyo. 

Taarifa iliyotolewa na Kamati ya Umoja inayoshughulikia masuala ya umoja wa Korea mbili ya upande wa Korea Kaskazini sambamba na kulaani hatua hiyo ya Korea Kusini na Marekani ya kufanya luteka ya pamoja ya kijeshi katika eneo hilo, imesema kuwa serikali ya Seoul, imeenda kinyume na maridhiano ya pande mbili na kwamba harakati hizo zimeikatisha matumaini serikali ya Pyongyang.

Chanzo: parstoday.com