http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html
Showing posts with label Museveni: Nchi za Afrika zinapaswa kuondoa ukomo wa kuwania urais. Show all posts
Showing posts with label Museveni: Nchi za Afrika zinapaswa kuondoa ukomo wa kuwania urais. Show all posts

Monday, May 13, 2019

Museveni: Nchi za Afrika zinapaswa kuondoa ukomo wa kuwania urais

Na RFI Imechapishwa 13-05-2019 Imehaririwa 13-05-2019 Saa 09:4

Mwezi mmoja baada ya Mahakama ya Juu nchini Uganda kuunga mkono hatua ya bunge kuondoa ukomo wa kuwania urais nchini humo, rais Yoweri Museveni anataka mataifa ya Afrika yaondokane na sheria zinazowazuia viongozi wenye umri mkubwa kuwania urais katika nchi zao.

media
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amesea yuko tayari kuwania katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2021. Capture d'écran al-Jazeera

Rais Yoweri Museveni wa Uganda anataka nchi za Afrika kukubali kubadlisha katiba zao kuondoa vizuizi vinavyowakataza viongozi wenye umri mkubwa na wale ambao wametawala kwa muda mrefu kuwania urais.

Rais Yoweri Museveni amesema kwamba ukomo uliowekwa kwenye katiba kama vile ukomo kwa mihula na ukomo kwenye umri vinazuia Afrika kuwa na viongozi wazuri na wenye uzoefu.

Rais Museveni anajiandaa kuwania katika uchaguzi wa urais mwaka 2021 na

akishinda, atakuwa mmoja wa viongozi wa Afrika waliotawala muda mrefu zaidi (miaka 40).

Bunge la Uganda limebadilisha katiba mara mbili na kumpa nafasi Museveni

kuwania kwenye kiti cha urais. Mnamo mwaka 2005, bunge liliondoa ukomo wa mihula na mwaka 2017 likaondoa ukomo wa umri wa miaka 75 nakumpa nafasi

Museveni kuwania kwenye kiti cha urais mwaka 2021.

Chanzo: sw.rfi.fr