Mkuu wa polisi ya mipaka nchini Marekani, John Sanders, ametangaza kuachia ngazi baada ya kugundulika kwamba watoto wahamiaji wanazuiliwa katika mazingira mbaya, hali ambayo ilifichuliwa kwa vyombo vya habari.
Mkuu wa polisi ya mipaka Marekani, John Sanders, ametangaza kujiuzulu kwenye nafasi yake ifikapo Julai 5. REUTERS/Jonathan Ernst
Katika ujumbe kwa maafisa wake, Kaimu Mkuu wa polisi wa mipaka nchini Marekani John Sanders ametangaza kwamba atajiuzulu kwenye nafasi yake Julai 5.
Tangazo la kujiuzulu kwake linakuja siku chache baada ya shirika la kimataifa la Haki za Binadamu Human Right Watch kuchapisha ripoti mbaya kuhusu hali ya watoto 250 waliotengwa na familia zao wanazuiliwa katika kituo cha Clint, karibu na El Paso, huko Texas.
"Watoto walipofika kwenye chumba cha mkutano, hatukuamini macho yetu," Warren Binford, mmoja wa wanasheria waliokutana na watoto hao, amesema katika mahojiano na kituo cha MSNB.
Walikuwa wagonjwa, walipungua kimwili, walikuwa wachafu sana, na haraka walianza kutuzungumzia kuhusu jinsi wanavyohisi njaa.
"Walieleza madhila mbalimbali yanayowakumba tangu kuzuiliwa katika kituo hicho, amesema Warren Binford.
"Ushuhuda wa wanasheria umezua hisia mbalimbali nchini. Siku ya Jumatatu usiku watoto walihamishwa, lakini Jumanne hii wiki hii, watoto mia moja walilazimishwa kurudi kwenye kituo hicho, kwa kukosa nafasi mahali pengine, amearifu mwandishi wetu huko Washington, Anne Corpet.
