Tunamuomba MOLA wetu Aliyetukuka na Mweza, katika mwezi huu wa Shawwaal 1440H Atujaalie furaha, amani, mapenzi, siha, iymaan, taqwa, ikhlaasw pamoja na karama na utukufu katika masiku yote ya uhai wetu.
Na bila ya kuwasahau kwa DU'AA zetu WATU wote waliopo kwenye dhiki, vita, ukandamizwaji, njaa, maradhi na wanaodhulumiwa pote duniani.
Tukimuomba *ALLAAH (Subhaanahu wa Ta’aalaa)* Awakwamue na kuwapa faraja na nusra. Tunamuomba *ALLAAH (Subhaanahu Wa Ta'aalaa)* Atutakabalie DU'AA zetu na za Waislam wote duniani, Aamiyn
*@Mswahiliflani Washington D.C*































