http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html
Showing posts with label Maandamano makubwa dhidi ya Baraza la Kijeshi Sudan yanafanyika tena leo. Show all posts
Showing posts with label Maandamano makubwa dhidi ya Baraza la Kijeshi Sudan yanafanyika tena leo. Show all posts

Friday, May 3, 2019

Maandamano makubwa dhidi ya Baraza la Kijeshi Sudan yanafanyika tena leo

Maandamano makubwa dhidi ya Baraza la Kijeshi Sudan yanafanyika tena leo
Mandamano makubwa ya kulishinikiza Baraza la Kijeshi nchini Sudan likabidhi uongozi na madaraka ya nchi kwa raia yanafanyika leo katika miji mbalimbali ya nchi hiyo.

Maandamano hayo yaliyoitishwa na muungano unaojulikana kwa jina la Vikosi vya Uhuru na Mabadiliko yanataka Baraza la Kijeshi la Sudan litkabidhi haraka mamlaka ya nchi kwa utawala wa kiraia.

Maandamano hayo yaliyoanza asubuhi ya leo katika mji mkuu wa Sudan Khartoum na miji mingine ya nchi hiyo yana nara isemayo: Maandamano ya Mamilioni ya Serikali ya Kiraia.

Muungano huo aidha umewataka wananchi wa Sudan kujitokeza kwa wingi Ijumaa ya leo kushiriki katika maandamano hayo ili kushinikiza kupatikane utawala wa kiraia.

Vikosi vya usalama nchini Sudan vinaonekana vikifunga baadhi ya barabara za mji mkuu Khartoum ili kuwazuia waandamanaji hao wasielekee upande waIkulu ya Rais.

Omar Hassan al-Bashir Rais wa zamani wa Sudan

Makundi ya kisiasa nchini Sudan yanalituhumu Baraza la Kijeshi la Mpito kwamba linakusudia kuendelea kushikilia madaraka kwa kisingizio cha kudhamini usalama wa nchi hiyo.