http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html
Showing posts with label Jakaya Kikwete: Licha ya juhudi kubwa za viongozi wa Afrika bado kuna matatizo makubwa ya kiutawala. Show all posts
Showing posts with label Jakaya Kikwete: Licha ya juhudi kubwa za viongozi wa Afrika bado kuna matatizo makubwa ya kiutawala. Show all posts

Thursday, May 23, 2019

Jakaya Kikwete: Licha ya juhudi kubwa za viongozi wa Afrika bado kuna matatizo makubwa ya kiutawala

Jakaya Kikwete: Licha ya juhudi kubwa za viongozi wa Afrika bado kuna matatizo makubwa ya kiutawala
Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa licha ya kuwepo juhudi chanya za viongozi wa Afrika kuonyesha ubunifu wa mipango ya maendeleo, lakini bado kuna tatizo la utawala.

Kikwete ameyasema hayo katika kongamanola 11 la kitaaluma la Mwalimu JK Nyerere lililofanyika Chuo Kikuu cha jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine amesema kuwa, licha ya Umoja wa Afrika (AU) kufanikiwa katika malengo yake ya kuleta uhuru kwa nchi wanachama, bado kuna changamoto tatu tatu ambazo ni kukosekana kwa utawala bora, umasikini na magonjwa. Aidha ameongeza kwa kusema; “Kumekuwa na changamoto zinazohitaji kuangaliwa ambazo ni kuwepo kwa sheria kandamizi, ushiriki usioridhisha wa wananchi, kutokuwepo kwa uhuru wa habari na kutokuwepo kwa mikakati ya kupambana na rushwa."

Eneo la Pembe ya Afrika na Afrika Mashar8iki

Kwa mujibu wa rais huyo wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, watu wa Afrika hawana njia nyingine, isipokuwa kutatua changamoto hizo za utawala. Mbali na utawala bora, Kikwete amesema kuwa bara la Afrika bado linatawaliwa na umasikini mkubwa na kwamba kati ya nchi 27 maskini zaidi duniani, 25 zipo Afrika. Ameongeza kwamba kuna mikakati mbalimbali imefanywa ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa mpango mpya wa ushirikiano wa kiuchumi (NEPAD).

Mbali na umaskini, amesema kuwa bara la Afrika bado linakabiliwa na magonjwa na kuutaja ugonjwa wa malaria kuwa tishio kubwa zaidi. Aidha amesema: “Sina uhakika kama viongozi wa Afrika walikuwa wakisikiliza maoni ya wengine kuhusu utawala bora." Amesema Kikwete.

Chanzo: parstoday.com