http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html
Showing posts with label Idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Sudan yafikia 60. Show all posts
Showing posts with label Idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Sudan yafikia 60. Show all posts

Wednesday, June 5, 2019

Idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Sudan yafikia 60

Na Victor Melkizedeck Abuso Imechapishwa 05-06-2019 Imehaririwa 05-06-2019 Saa 11:13

Watu waliopoteza maisha kwa kupigwa risasi na wanajeshi nchini Sudan, baada ya kambi ya waandamanaji kuvunjwa siku ya Jumatatu imefikia 60.

media
Wanajeshi walivyosambarataisha kambi ya waandamanaji jijini Khartoum nchini Sudan
ASHRAF SHAZLY / AFP

Takwimu hizi zimetolewa na Madaktari nchini humo lakini pia makundi ya wanasiasa wa upinzani ambayo yamelaani mauaji hayo.

Ripoti zinasema kuwa, wanajeshi wanafanya ziara katika barabara za jiji la Khartoum, kuhakikisha kuwa hakuna waandamanaji wanaonekana.

Machafuko yalizuka siku ya Jumatatu, baada ya jeshi kuamua kuvunja kambi ya wakimbizi waliokuwa wanaendelea kushinikiza jeshi kukabidhi madaraka kwa raia.

Hatua hiyo imelaaniwa vikali na mataifa ya Magharibi lakini Urusi na China zimezuia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kulaani mauaji yaliyotokea nchini Sudan.