http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html
Showing posts with label Guterres ataka uchunguzi huru wa kushambuliwa meli za mafuta Bahari ya Oman. Show all posts
Showing posts with label Guterres ataka uchunguzi huru wa kushambuliwa meli za mafuta Bahari ya Oman. Show all posts

Saturday, June 15, 2019

Guterres ataka uchunguzi huru wa kushambuliwa meli za mafuta Bahari ya Oman

Guterres ataka uchunguzi huru wa kushambuliwa meli za mafuta Bahari ya Oman
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa mwito wa kufanyika uchunguzi huru wa tukio la kushabuliwa meli za mafuta katika Bahari ya Oman.

Antonio Guterres amesema uchunguzi huru tu ndio unaweza kubaini ukweli kuhusu tukio hilo la Alkhamisi. Amesema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ndicho chombo chenye mamlaka ya kuagiza uchunguzi wa shambulizi hilo.

Katibu Mkuu wa UN ameeleza bayana kwamba: "Ni muhimu tujue ukweli kuhusu shambulizi hilo na ni muhimu pia kuweka wazi majukumu ya kila taasisi. Hilo linaweza tu kubainika iwapo kuna taasisi huru ya kutathmini ukweli kuhusu tukio hilo."

Hii ni katika hali ambayo, Rais Donald Trump katika mahojiano na kanali ya televisheni ya Fox na bila kutoa ushahidi wowote, alidai kuwa Iran imehusika na shambulizi hilo.

Moshi ukifuka kutoka kwenye meli za mafuta zilizoshambuliwa


Aidha Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amedai kuwa Iran imehusika na hujuma hiyo, kwa kutegemea video bandia iliyobuniwa na maafisa wa serikali ya Washington. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekanusha vikali madai hayo yasiyo na msingi.


Alkhamisi iliyopita vyombo vya habari viliripoti kujiri shambulizi dhidi ya meli mbili za mafuta zilizokuwa zimebeba mafuta ghafi katika Bahari ya Oman, ambapo Jeshi la Majini la Iran liliwaokoa mabaharia wa Kirusi waliokuwa kwenye meli hizo.

Chanzo: parstoday.com