http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html
Showing posts with label Algeria mtanange wa kukatana shoka. Show all posts
Showing posts with label Algeria mtanange wa kukatana shoka. Show all posts

Saturday, July 13, 2019

Nigeria, Algeria mtanange wa kukatana shoka

Na MASHIRIKA

CAIRO, Misri: Baada ya kuwabandua Ivory Coast 4-3 kupitia kwa mikwaju ya penalti Alhamisi usiku, Algeria wanaopigiwa upatu wa kutwaa taji la mwaka huu watakutana na Nigeria kesho Jumapili katika nusu-fainali, kuanzia saa nne usiku.


Nusu-fainali ya kwanza itakutanisha timu za Senegal na Tunisia kuanzia saa mbili usiku.

Baghdad Bounedjah aliifungia Algeria bao katika muda wa kawaida kabla ya Johanthan Kodjia kusawazishia Ivory Coast.

Wakati wa penalti, Youcef Belaili wa Algeria alipoteza penalti yake kwa kupiga mwamba wa goli, sawa na Serey Die wa Ivory Coast.

Bounedjah alikuwa amepoteza penalti awali katika muda wa kawaida na kuwapa wasiwasi mashabiki wa timu yake ambao wamesubiri ubingwa wa taji hili tangu waunyakue kwa mara ya mwisho mnamo 2010.

Ni mechi ambayo Ivory Coast walitawala kwa kiasi kikubwa hasa katika kipindi cha kwanza, huku kipa Rais Mbolhi akikumbwa na wakati mgumu wa kupangua makombora ya washambuliaji wa timu hiyo kutoka Afrika Magharibi.

Wakati huo huo, kocha Pep Guardiola wa Manchester City ameeleza kufurahishwa kwake na kiwango cha winga wake, Riyad Mahrez ambaye timu yake ya Algeria imetinga hatua ya nusu-fainali ya AFCON.

Guardiola anayejiandaa kuwakaribisha wachezaji wake kwa maandalizi ya msimu mpya alisema kiwango cha Mahrez kimeimarika zaidi nchini hapa, huku akimtarajia kukiendeleza zaidi atakaporudi klabuni.

Ushindani

Klabuni, Mahrez anashindania namba dhidi ya Leroy Sane, Raheem Sterling na Bernardo Silva.