Shukran zetu za dhati tunziandika hapa leo, kwa kaka zengu hawa wapendwa, khususan kwa Brother Sabri Zungu, ambae ni huyo wakwanza upande wetu wa kulia, tukiwa na kaka yetu mpendwa, Waheed AL FARSY katikati Wow
Kaka Subri Zungu ni mmoja alietuandali mahojiano yetu ya Swahili Villa Online TV & America Swahili News na Abdullah Juma Aley A.K.A Abdulwakati Bin Juma, ambae ni Mchezaji Mkubwa Nyota isiyosahaulika katika fani ya soka na mpira wa meza ( Table tennis) kwenye miaka ya 1970 - 1990 - Ndani na njee ya Zanzibar
Hizi ni shukurani zetu kwa upendo wao mkubwa waliotuonyesha kwetu, kwakweli tunashukuru Interview imeenda Viral na imetujengea heshima kubwa ya kuzidi kuwapenda na kuwaenzi wale wote waliofanya vyema kwaajili ya Nchi yetu, tunawajua na wanajulikana kuutokana na vipaji vyao na uwezo waliobarikiwa.
Kwahilo tunaowaomba Wadau wetu wanaotufatilia katika Channel yetu, ushirikiano mkubwa wa kutupa mawazo zaidi ili tupate kujifahari kama wananchi tunaojitolea kwaajili ya mapenzi ya Nchi yetu, kazi ya media ni ngumu sana na haswa wale wanaojitolea kwaajili ya utu bila ya kuthamini kitu, hapa ndipo inapopatikana baraka na thamani juu ya kile unachokifanya.
Kwa hiyo sisi tunawaomba ushirikiano mkubwa kutoka kwenu, usione tabu wa ku-Sambaza video zetu kwenye platforms yako, na make sure: una - subscribe, Channel zetu, like share kwenye ukurasa wako, comments ikiwezekana katika Channel zetu hizo.!
Bila ya kuwasahau Nyuma ya Camera | Ashuru- Abuu Magoma.
Tunatanguliza Shukurani & Much Love
Abou-Shatry’s | Washington, DC Studio Producer


Sambaza UPENDO kwa wote Nasi tunawapenda Sana

No comments:
Post a Comment