http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html

Wednesday, May 26, 2021

Wasiwasi wa WHO kuhusu ugavi usio wa kiadilifu wa chanjo ya corona

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameashiria ugavi usio wa kiadilifu wa chanjo ya corona duniani na kusema kuwa anatiwa wasiwasi na uhaba wa chanjo hiyo katika baadhi ya nchi maskini duniani. Akihutubia kikao cha shirika hilo, Dakta Tedros Adhanom amekosoa mchakato wa utoaji chanjo unaoendelea sasa duniani na kueleza kuwa, suala hilo limesababisha kuongezeka maambukizi ya corona.

Amesema zaidi ya asilimia 75 ya chanjo zote za corona zimegawiwa kwa nchi 10 pekee. Ugavi wa chanjo ya corona usio wa kiadilifu Dakta Adhanom amesisitiza kuwa, baada ya kupita karibu miezi 18 tangu kuibuka janga la corona liloathiri sekta ya afya duniani, dunia ingali ipo katika hali mbaya. Amesema licha ya hali ya sasa ya janga la corona idadi ya vifo wiki tatu zijazo itaongezeka na kupindukia ile ya mwaka jana. 

Ugavi wa chanjo ya corona usio wa kiadilifu

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameongeza kuwa, hakuna njia yoyote ya kubainisha kidiplomasia suala hili na kwamba hatima ya dunia nzima iko mikononi mwa nchi chache ambazo zina jukumu la kuzalisha chanjo nyingi za ugonjwa wa corona. 

Takwimu za WHO zinaonyesha kuwa, hadi sasa watu milioni 167,593, 596 wameambukizwa corona duniani kote na wengine milioni tatu na 479,925 wameaga dunia kwa ugonjwa huo.



No comments:

Post a Comment