http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html

Friday, November 22, 2019

Schiff: Mwenendo wa Trump mbaya kuliko wa Nixon

Image result for Adam Schiff
Mwenyekiti wa kamati ya bunge nchini Marekani Adam Schiff

Mwenyekiti wa kamati ya bunge nchini Marekani inayosikiliza ushahidi katika mchakato wa kutaka kumshitaki Rais Donald Trump, Adam Schiff, amesema mwenendo wa Rais Trump na Ukraine ulikuwa mbaya zaidi, kuliko yale yaliyosababisha kuanguka kwa Rais Richard Nixon.

Adam Schiff amesema hayo wakati wa kumalizika kwa vikao vya kusikiliza ushahidi kuhusu tuhuma zinazomkabili Rais Trump kuwa alitumia mamlaka yake vibaya kwa manufaa yake binafsi kisiasa, kwa kutaka Ukraine ifanye uchunguzi dhidi ya mpinzani wake wa kisiasa Joe Biden.

Hayo yakijiri, Rais Trump amesema anataka kesi ya kushtakiwa bungeni, ipelekwe katika baraza la Seneti kwa sababu huko kutakuwa na haki na utaratibu mzuri.

Aidha, Trump amesema anatarajia kuwa mgombea wa kiti cha urais wa chama cha Democratic Joe Biden, atakuwa miongoni mwa mashahidi.

Via .dw.com

No comments:

Post a Comment