http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html

Thursday, July 18, 2019

Bunge la Marekani lazuia mauzo ya silaha kwa Saudia, Trump kutumia veto

Bunge la Marekani lazuia mauzo ya silaha kwa Saudia, Trump kutumia veto
Bunge la Wawakilishi la Marekani limepiga kura kuunga mkono maazimio ya kupinga mauzo ya silaha zenye thamani ya mabilioni ya dola kwa Saudi Arabia.

Wabunge hao wamepasisha maazimio hayo ya kuzuia mauzo ya silaha kwa Saudia, yakiwemo makombora erevu ya kuelekezwa ya (PGMs) licha ya vitisho vya Rais Donald Trump aliyedai kuwa atatumia kura ya turufu kupinga hatua hiyo ya Wabunge wa Kongresi.

Maazimio mawili kati ya yaliyopasishwa yamepigiwa kura 238, huku thuluthi moja ya maazimio hayo ikiungwa mkono kwa kura 237.

Mbunge wa chama cha Democratic, Eliot Engel ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Kigeni ya Bunge hilo amesema, "Kupasishwa maazimio hayo kwa kuungwa mkono na pande hasimu za kisiasa kunatuma ujumbe wa wazi kwamba thamani zetu lazima ziongoze sera zetu za kigeni."

Haya yanajiri mwezi mmoja baada ya Bunge la Seneti la Marekani kupiga kura ya kuunga mkono maazimio 22 ya kupinga mauzo ya silaha zenye thamani ya dola bilioni 8.1 kwa Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Jordan yaliyoidhinishwa hivi karibuni na utawala wa Trump bila idhini ya Kongresi.

Wanaharakati wakipinga mauzo ya silaha kwa Saudia

Mei mwaka huu, Rais Donald Trump alidai kuwa, taharuki katika eneo imeshadidishwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwamba mauzo ya silaha hizo yatawasaidia na kuwadhaminia usalama waitifaki wa Washington na kuimarisha uthabiti katika eneo la Asia Magharibi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo kwa upande wake alidai kuwa, "Mauzo ya silaha kwa Saudia, Imarati na Jordan yakiwemo makombora erevu ya kuelekezwa ya (PGMs) hayawezi kucheleweshwa zaidi, wakati huu ambapo taharuki imeongezeka katika eneo."

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment