http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html

Tuesday, June 18, 2019

Umoja wa Ulaya umetaka kufanyika uchunguzi huru kuhusu machafuko Sudan

Umoja wa Ulaya umetaka kufanyika uchunguzi huru kuhusu machafuko Sudan
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya wametaka kufanyika uchunguzi huru na wa wazi kuhusu kukandamizwa wafanya maandamano nchini Sudan.

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya wamelaani mashambulizi ya utumiaji mabavu huko Sudan yaliyoplekea kuuawa na kujeruhiwa idadi kubwa ya raia. Mawaziri hao wamesema kuwa Baraza la Kijeshi la Uongozi wa Mpito Sudan linahusika na machafuko hayo. 

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya walibainisha hayo jana mwishoni mwa kikao chao huko Luxembourg. Katika upande mwingine, mirengo saba ya kisiasa nchini Sudan kwa jina la Muungano wa Makundi ya Kitaifa pia imetaka kuundwa serikali ya mpito nchini humo.

Baraza la kijeshi la Sudan


Mawaziri hao wa Umoja wa Ulaya wametaka kusitishwa machafuko khussan vitendo vya kuwanyonga watu kidhulma na nje ya fremu ya kisheria. 

Mirengo hiyo ya kisiasa Sudan imepinga uingiliaji wa nchi ajinabi katika masuala ya ndani ya nchi yao na kulitolea wito Baraza la Kijeshi linaloongoza nchi kufuta hukumu ya kuwanyonga wanaharakati wa kisiasa na viongozi wa vyama mbalimbali ili kuandaa uwanja wa kufanyika mazungumzo.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment