http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html

Friday, June 28, 2019

China yataka kuwepo mwafaka wa kimataifa wa kukabiliana na sera za mabavu za Marekani

China yataka kuwepo mwafaka wa kimataifa wa kukabiliana na sera za mabavu za Marekani
Mwakishi wa kudumu wa China katika jumuiya za kimataifa mjini Vienna ametoa wito wa kuwepo mwafaka wa kimataifa wa kukabiliana na hatua za kutumia mabavu na siasa za kujichukulia maamuzi ya upande mmoja za Marekani.

Wang Qun ameliambia kongamano la kimataifa mjini Vienna huko Austria kwamba, siasa za kutumia mabavu na sera za kujichukulia maamuzi ya upande mmoja ni ukiukaji wa hati ya Umoja wa Mataifa na sheria na kanuni za kimataifa na inaonekana kuwa, baadhi ya nch zinatumia njia hiyo kwa ajili ya kufikia malengo yao.

Mwakilishi wa kudumu wa China amesema kuwa, kama Marekani haiwezi kutumia sheria za kimataifa kwa ajili ya kutimiza malengo yake basi inapaswa kutegemea sheria zake za ndani na kanuni za kiserikali.

Donald Trump

Wang Qun ameongeza kuwa Marekani inatumia vikwazo kama wenzo na fimbo ya kutekeleza siasa zake za mabavu. Hata hivyo amesisitiza kuwa siasa za vikwazo zinaidhuru pia nchi inayoziwekea nyingine vikwazo hivyo na kwamba uchunguzi umebaini kuwa, hatua ya serikali ya Donald Trump ya kuzidisha ushuru wa forodha imezidisha pia mzigo wa dola bilioni 69 kwa mwaka katika gharama na matumizi ya Wamarekani.

Mwakilishi wa China mjini Vienna amesema Beijing ambayo inakabiliana na sera za kutumia mabavu za Marekani inapinga suala la kuiwekea vikwazo nchi yoyote na inatetea utawala wa sheria za kimataifa.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment