Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa jana alimteuwa tena Tito Mboweni kuwa Waziri wa Fedha katika baraza lake jipya la mawaziri. Rais Ramaphosa amechukua hatua hiyo ikiwa ni ahadi alizotoa kabla ya uchaguzi kuelekea kutekeleza mageuzi, kufufua uchumi na kuvutia wawekezaji nchini humo.
Cyril Ramaphosa ambaye aliapishwa Jumamosi iliyopita kuwa Rais wa Afrika Kusini kwa kipindi cha kwanza kamili cha miaka mitano amepunguza idadi ya mawaziri katika baraza lake jipya kutoka 36 hadi 28.
Hatua hiyo imetajwa na wachambuzi wa mambo kuwa itatumika kama kipimo ambacho kitatathmini uwezo wake wa kuchochea mageuzi zaidi kupitia mabadiliko makubwa aliyoahidi kuyatekeleza tangu achukue hatamu za uongozi mwaka uliopita baada ya kujiuzulu Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma aliyekuwa akikabiliwa na tuhuma za ufisadi.

Akilihutubia taifa kwa njia ya televisheni, Rais wa Afrika Kusini amesema kuwa ameteuwa baraza hilo jipya la mawaziri ili kupunguza matumizi ya serikali. Amesema katika sekta na maeneo yote ya serikali wamekusudia kufufua uchumi wa nchi kwa kutumia kwa umakini mkubwa fedha za umma. Masoko yanatazamia kukaribisha uteuzi huo wa Mboweni; gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Afrika Kusini anayeshemiwa pakubwa na wawekezaji.
Tito Mboweni, Waziri mpya wa Fedha wa Afrika Kusini

No comments:
Post a Comment