Jeshi la polisi la New Zealand limetangaza habari ya kufunguliwa mashtaka rasmi ya ugaidi, raia wa Australia aliyefanya mauaji ya umati dhidi ya Waislamu katika mji wa Christchurch huko New Zealand sambamba na mashtaka mengine. Mashambulizi yaliyofanywa katika misikiti miwili ya mji wa Christchurch nchini News Zealand yalipelekea Waislamu 51 kuuawa shahidi na makumi ya wengine kujeruhiwa.
Shirika la habari la Reuters limetangaza habari hiyo na kulinukuu jeshi la polisi la New Zealand likisema kuwa, mshambuliaji huyo raia wa Australia amefunguliwa rasmi mashtaka ya kufanya vitendo vya kigaidi huko New Zealand.
Brenton Tarrant mwenye misimamo mikali ya kibaguzi anayefuata fikra za rais wa Marekani, Donald Trump za ubora wa watu weupe kuliko watu wengine wowote anakabiliwa pia na mashtaka mengine 51 ya mauaji na mashtaka mengine 40 ya kujaribu kuua.
Kesi ya gaidi huyo imepangwa kusikilizwa tena mwezi ujao wa Juni.
Katika shambulio hilo la Ijumaa ya Machi 15, 2018 kijana huyo mwenye chuki dhidi ya Uislamu ambaye alitangaza mwenyewe kuwa ni mfuasi wa rais wa Marekani Donald Trump, aliyarusha hewani mubashara mauaji hayo ya kinyama kupitia facebook na Youtube.
Watu wasiopungua 50 wakiwemo wanawake na watoto wadogo waliuawa na makumi ya wengine walijeruhiwa katika mashambulio ya kigaidi yaliyofanywa dhidi ya misikiti miwili katika mji wa Christchurch nchini New Zealand wakati waumini wakiwa wamekusanyika kwa ajili ya Sala ya Ijumaa.
Chanzo: parstoday.com

No comments:
Post a Comment