Wananchi wa Afrika Kusini zaidi ya milioni 26 wameajiandikisha kushiriki uchaguzi huo wa leo ambapo kwa kiasi kikubwa chama tawala cha ANC kinatazamiwa kuibuka na ushindi.
Uchaguzi wa leo unahesabiwa kuwa na umuhimu mkubwa kwa wananchi wa Afrika Kusini baada ya nchi yao kukabiliwa na sakata mbalimbali za ufisadi kwa miaka kadhaa ndani ya chama tawala ANC. Wapiga kura wasiopungua milioni 26.8 wamejiandikisha kupiga kura katika vituo 22,925 kote nchini humo. Vituo hivyo vimefunguliwa kuanzia saa moja asubuhi kwa wakati wa huko na vinatazamiwa kufungwa masaa 14 baadaye.
ANC, chama tawala cha Afrika Kusini
Matokeo ya awali yatatangazwa kesho; na mshindi rasmi atatangazwa Jumamosi ijayo. Itakumbukwa kuwa, nchini Afrika Kusini chama ambacho kitaibuka na ushindi wa viti vingi bungeni ndicho kitakachomchagua rais ambaye ataaapishwa tarehe 25 mwezi huu. Makumi ya vyama vinachuana katika uchaguzi wa rais na bunge wa leo huko Afrika Kusini huku vyama vikuu vinavyochuana vikali vikiwa ni chama tawala cha ANC, chama cha the Economic Freedom Fighter (EFF) na chama cha the Democratic Alliance (DA).
Chanzo: parstoday.com

No comments:
Post a Comment