http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html

Friday, April 12, 2019

Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini: Lazima mazungumzo kati ya Trump na Kim Jong-un yaendelee

Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini: Lazima mazungumzo kati ya Trump na Kim Jong-un yaendelee
Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini ametaka kuendelezwa mazungumzo kati ya Marekani na Korea Kaskazini kwa ajili ya kutatua mzozo wa eneo la Rasi ya Korea.

Rais Jae-in ameyasema hayo katika mazungumzo yake na Rais Donald Trump wa Marekani mjini Washington ambapo pamoja na mambo mengine ametaka kuendelezwa duru ya tatu ya mazungumzo kati ya rais huyo wa Marekani na Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini. 

Amesema kuwa mzozo wa eneo la Rasi ya Korea unaweza kutatuliwa tu kwa kupitia njia ya mazungumzo, huku akionyesha kupungua mvutano wa kijeshi katika eneo hilo ikilinganishwa na kipindi cha huko nyuma. Hii ni katika hali ambayo katika mazungumzo hayo Rais Donald Trump pia amesema kuwa, Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini amekubali kununua zana zinazohitajika za kijeshi za Marekani kwa ajili ya nchi yake.

Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini akiwa na Trump

Mkutano wa pili kati ya Trump na Kim Jong-un wa Korea Kaskazini ulifanyika kati ya tarehe 27 na 28 ya Februari mwaka huu mjini Hanoi, Vietnam ambapo ulimazika bila kufikiwa natija yoyote. Viongozi wa Korea Kaskazini walitangaza kwamba hatua ya kupenda makubwa ya rais huyo wa Marekani ndio iliyopelekea mazungumzo hayo kuvunjika. Hii ni katika hali ambayo duru ya kwanza ya mazungumzo ya viongozi hao ilifanyika tarehe 12 Juni mwaka jana nchini Singapore ambapo licha ya kutiliana saini makubaliano kadhaa, lakini upande wa Marekani haukutekeleza hata kidogo makubaliano tajwa, suala ambalo daima limekuwa likilaaniwa vikali na viongozi wa Korea Kaskazini.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment