Korea Kaskazini inataka kuondolewa waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo, kutoka kwa mazungumzo ya nyuklia ikimlaumu kwa kuzungumza mambo yasiyo ya maana na pia kwa kuzungumza kiholela.

Pompeo ashafanya mkutano na Kim Jong un
Afisa wa wizara ya mashauri ya kigeni alisema kuwa mazungumzo zaidi hayatakwenda vizuri ikiwa Pompeo atahusika, akitaka kuwepo mtu muangalifu zaidi kuchukua mahala pake.
Hii inakuja baada ya Korea Kaskazini kusema ilikuwa imefanyia majaribio silaha mpya.
Jaribio hilo ndilo la kwanza tangu mkutano wa mwezi Februari mjini Hanoi kati ya viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini umalizike bila makubaliano.
Bw Pompeo alizuru Korea Kaskazini mara nne mwaka uliopita ikiwemo wakati wa mkutano kati yake na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Chanzo: nipasheonline.com

No comments:
Post a Comment