http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.html

Friday, April 26, 2019

Kim Jong-un: Marekani imekuwa na miamala ya upande mmoja katika mazungumzo

Kim Jong-un: Marekani imekuwa na miamala ya upande mmoja katika mazungumzo
Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini amesema kuwa, kupatikana amani eneo la Rasi ya Korea kunategemea mienendo ya Marekani.

Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini ameyasema hayo katika mazungumzo yake na Rais Vladmir Putin wa Russia, katika mji wa Vladivostok wa nchi hiyo na kubainisha kwamba, katika mazungumzo ya Februari mwaka huu mjini Hanoi, Vietnam, Rais Donald Trump wa Marekani alichukua mienendo na upande mmoja. Aidha Kim Jong-un amesema kuwa hali ya sasa katika eneo la Rasi ya Korea ni mbaya. 

Kiongozi huyo kijana aliwasili Russia Jumatano kwa ajili ya kukutana na kufanya mazungumzo na rais wa nchi hiyo ambapo ameyataja mazungumzo ya pande mbili na Rais Vladmir Putin kuwa ya kirafiki.

Trump ambaye hufuata misimamo ya upande mmoja katika mazungumzo na Kim Jong-un


Shirika la Habari la Korea Kaskazini limesema kuwa, Kim Jong-un amempa mwaliko rasmi Rais Putin kufanya safari mjini Pyongyang ambapo naye amekubali mwaliko huo. 

Aidha viongozi hao wa Korea Kaskazini na Russia mjini Vladivostok wamekubaliana kuinua kiwango cha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi katika ngazi ya juu. Hii ni mara ya kwanza kwa Kim Jong-un kufanya safari nchini Russia.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment