Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lu Kang, ametupilia mbali ukosoaji wa Marekani kuhusiana na siasa za Beijing kulihusu eneo la Amerika ya Latini.
Sambamba na kukanusha madai ya Washington kuhusiana na msimamo wa China katika eneo la Amerika ya Latini Lu Kang amesema kuwa, msimamo wa viongozi wa Marekani juu ya uhusiano wa China na nchi za Amerika ya Latini, ni wa kudhalilisha, uchochezi na wa kukimbia majukumu. Ameongeza kwamba kwa muda mrefu Marekani ilikuwa emelifanya eneo la Amerika ya Latini kuwa bustani yake ya kujifaragua sambamba na kuziwekea mashinikizo na vitisho nchi nyingine, na hata kufikia kuzing'oa madarakani serikali za eneo hilo.
Urafiki wa China na Venezuela waitia kiwewe Marekani
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amezidi kufafanua kuwa nchi za Amerika ya Latini sasa zimefahamu kwamba ni nani rafiki yao wa kweli. Itakumbukwa kuwa Ijumaa iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo na akiwa katika safari yake ya siku tatu katika nchi za Chile, Paraguay na Peru aliituhumu China kwamba imechangia kuporomoka kwa uchumi wa Venezuela kwa kumuunga mkono kifedha Rais Nicolás Maduro wa Venezuela. Aidha Pompeo ameituhumu China kwa undumakuwili na kutokuwa na uaminifu.
Chanzo: parstoday.com

No comments:
Post a Comment